KANUNI SAHIHI ZA KILIMO BORA CHA MACHUNGWA
Mchungwa ni jamii ya mlimao, lakin hustawi zaidi ukanda wa pwani wenye joto kiasi, mvua zaidi na udongo wenye rutuba. Hapa Tanzania mikoa kama Pwani, Dar es salaam, Tanga, Mtwara, Lindi, na Morogoro ni maarufu kwa kilimo hiki. Pia tunda la mchungwa huliwa na binadamu ili kuongeza vitamini mwilini. HALI YA HEWA Michungwa huweza kukuzwa maeneo yenye joto na hata yale yenye baridi. Kama ilivyo kwa matunda mengineya citrus, ili kupata mazao mazuri haina budi kukuza michungwa katika joto la nyuz ijoto 15.5c – 29c. KUANDAA MBEGU Mchungwa kwa kuanzia unakusanya mbegu za mlimao kutoka katika malimao yaliyokomaa na ikiwezekana yawe yameiva yakiwa mtini, kausha mbegu zake na kasha unaweza kutolea ganda la nje ili ziweze kuota vizuri. KUANDAA KITALU Tengeneza kitalu chako vizuri kwa kutumia jembe, kisha changanya na mbolea za mboji au samadi baada ya kukauka vema mwaga mbegu zako na uzifukie kwa udongo kiasi cha nusu sentimita, kasha mwagia maji kila siku na baada ya wiki 3...