Kilimo Bora Cha Matikiti Maji

Matikiti maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wastani. Zao hili lina wapatia watu shughuri za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi. Matikiti maji ni mojawapo ya jamii aina ya matunda au mbogaboga inayotambaa.

Mbegu Bora za Matikiti 
Mbegu maarufu ya tikiti ni Sukari F1, hata hivo madukani zinapatikana nyingi bora na tofauti tofauti kama vile:
  • Arashani F1 – kutoka Syngenta 
  • Sukari F1 – Kutoka East Africa seeds 
  • Sugar king F1 – kutoka Africasia 
  • Juliana F1 – kutoka Kiboseed 
  • Zebra F1 – Kutoka Balton 
  • Pato F1 – Kutoka Agrichem

MAHITAJI YA TIKITIMAJI

Tikiti linakua vizuri katika udongo unaoshika maji vizuri lakini yasio tuama na kuruhusu mzunguko mzuri wa hewa na maji.Udongo wenye pH 5.8-6.6.pia kama pH ni ndogo tutakushauri cha kufanya ili iweze kuwa nzuri na ya kiasi kwa ajili tikitimaji. Tikiti halistawi vyema ktk baridi na linahitaji joto la udongo kiasi cha 18-29 0c. Joto chini ya 18 0c na juu 29 0c litaathiri kuota kwa mbegu na ukuaji wa mmea.Katika kipindi cha ukuwaji tikitimaji linahitaji unyenyevu wa udongo wakati wote lakini maji yakizidi katika udongo wakati wowote wa ukuwaji na uwekaji wa matunda hupelekea upasukaji wa matunda na kupunguza mavuno na ubora wa matunda.

Upandaji wa tikiti maji
Katika shamba la ukubwa wa hekta moja kiasi cha kilo 3 – 4 cha mbegu kinaweza kutumika. Panda mbegu 2 au 3 moja kwa moja katika kila shimo. Usipande katika kitalu kwasababu miche ya mitikiti huwa ni dhaifu sana wakati wa upandikizwaji iwapo itapandwa kwenye kitalu hivyo kupelekea kufa kwa miche hiyo. Panda umbali wa sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa mita 1 hadi 2 kutoka shina hadi shina na mita 1.5 – 3 kutoka mstari hadi mstari. 

Zingatia: usitumie mbegu za tikiti ulilonunua (kwa ajili ya kula) kwasababu linaweza kuwa ni chotara (Hybrid) ambayo hupelekea kushusha kiasi na ubora wa matikiti yatakayo zaliwa kwa sababu yatakuwa ni kizazi cha pili (F2).


Mahitaji ya Mbolea ya Matikiti Maji
·         Mbolea ya kupandia: Wakati wa kupanda tumia DAP weka gram 5 kwa kwa kila shimo (lenye mbegu moja, na weka gram 10 au 15 kama kuna mbegu 2 au 3), hakikisha mbolea na mbegu havigusani.

·     Mbolea ya kukuzia: Wiki mbili baada ya miche yako kuota weka mbolea ya kiwandani NPK (Yaramila winner) gram 5 tena kwa kila mche, hakikisha unaichimbia chini na isigusane na mmea.

Umwagiliaji 
Shamba linatakiwa limwagiliwe mara kwa mara wakati mvua zinapokosekana au wakati wa mvua chache. Kipindi muhimu zaidi ambapo mimea hii huhitaji maji ni katika kipindi cha uotaji wa mbegu, wakati wa kutoa maua na siku takribani kumi kabla ya kuvuna. Iwapo kutakuwa na ukosefu wa maji kutasababisha kutengenezwa kwa matunda ambayo si mazuri na yenye umbo baya, pia kupungua kwa ukubwa wa tunda.
Angalizo: usimwagilie matikiti wakati wa jioni sana au usiku kwasababu inaweza kusababisha magonjwa ya majani kutokana na unyevu kukaa muda mrefu. Vile vile usimwagilie juu ya maua wakati wa asubuhi au jioni kwasababu unaweza kuzuia wadudu kama nyuki ambao ni muhimu sana wakati wa uchavushaji. 
Mangonjwa 
1) Ubwiru chini (Downy mildew)
2) Ubwiru juu (Powdery mildew ) 

3) Kata kiuno.(Damping off)



Wadudu

1)Inzi wa matikiti
hawa wadudu ni waharibifu kweli kweli na uharibifu wake hufanywa usiku.Uwaribifu huanza kipindi matikiti yanapoanza kutoa mauwa na ndo kipindi muhimu tikiti kuanza kutoa vitoto.Nzi jike hutaga mayai katika tikiti dogo na kusababisha muozo ndani ya hilo tunda.

Jinsi ya kugundua kama umevamiwa na hao inzi
1.utaona doa/doti nyeusi mbili kwenye kitoto 



2.Utaona muozo na pia kudondoka kwa tikiti hilo

3.Husababosha tunda kuwa na umbo baya



JINSI YA KUZUI

Kuna njia nyingi tu ambazo zinafanya kazi vizuri sana katika kuwaondoa hawa..Katika kitabu changu cha KILIMO CHA TIKITIMAJI kimeeleza njia zinazo fanya kazi kwa aslimia 100 ya  jinsi ya kuwandoa hawa wadudu shambani kwako..Hicho kitabu kinapatikana kwa njia ya EBOOK tunakutumia kwa njia ya whatsapp..Jinsi ya kukipata tuma message au piga simu kwa namba 0769550328. 




1) Wadudu mafuta (Aphid)
Hawa hushambulia majani na kufyonza juis ya mmea na baada ya kushambulia majani hujikunja na baadaye kupelekea mangonjwa ya virusi.

Dawa yao.
Tafuta Actara na pulizia majani pamoja na udongo.

Wadudu wengine ni;Nzi weupe (whitefly )-Actara itawamaliza.

,Utitiri mwekundu (Redspidermites)-Dynamec itawamaliza,Thrips-Actara na Dynamec itawamaliza kabisa.

MCHANGANUO WA KIPATO CHA MATIKITI KWA UFUPI
Vitu vya kuzingatia:
  • Hekta 1 = Square meter 10,000
  • Ekari 1 = Square meter 4000
  • Hekta 1 = Ekari 2.5
Tuchukulie mathalani una ekali moja
Ukipanda matikiti yako kwa nafasi ya 1m x 2m utakua na mashimo 2000 ya kupanda mbegu zako. Ikiwa kila shimo utapanda mbegu tatu na ukapunguzia mche mmoja na kuacha miwili ikue basi utakua na mimea 2 x 2000 = 4000.

kwa hiyo kwa ekali moja utakua na mimea 4000 ya matikiti. haya tufanye umeipunguzia matunda na hivyo kuufanya kila mmea uzae matunda mawili tu hivyo tunatarajia utavuna matunda 2 x 4000 = 8000.

Hivyo basi katika ekali moja ya matikiti uliyopanda kwa nafasi ya 1m x 2m ukakuza mimea 4000 utapata matunda 8000!

Tuchukulie mathalani umeamua kuuza matikiti yako shambani kwa bei ndogo kabisa ya Tsh. 1000 kwa tikiti moja, ukiuza matikiti yote 8000 utapata jumla ya Tsh. 1000 x 8000 = Tsh. 8,000,000 (Milioni nane)! 

Inawezekana kabisa kuwa huu mchanganuo ni wa nadharia tu lakini ndugu yangu tumechukulia makadirio ya chini sana. Unajua ni kwanini? 
Angalia hapa: 
  • Mmea mmoja unaweza kuzaa matunda mangapi? We unajua lakini licha ya hayo yote sisi tumechukulia matunda mawili tu kwa mmea mmoja. 
  • Pia bei ya tikiti inategemea ukubwa wake lakini sisi tumechukulia yote ni sawa na tunauza kwa bei moja tu. 
  • Halafu pia bei ya matikiti tumechukulia ni Tsh 1000 tu wakati inaweza kuwa hadi Tsh 2000 uki-target wakati mzuri kwa soko
UKITAKA MAELEZO ZAIDI TUNA KITABU KINACHOHUSU KILIMO CHA TIKITIMAJI,WASILIANA NASI KWA NAMBA HAPO CHINI




kwa nini nakushauri uwe na kitabu hichi
1.utajifunza kuandaa shamba kitaalamu
2.utajifunza mbegu nzuri ya tikitimaji ambayo ipo sokoni kwa sasa
3.kama ujawahi lima utaona mchanganuo wa bajeti katika ekari 1
4.kama ujawahi lima utaweza kujua ratiba ya shambani ambayo inaeleza shughuli na siku sahihi
5.utajua jinsi ya kuzibiti wadudu na magonjwa yanayosumbua katika zao la tikiti
6.Utajua mbinu za kuongeza mavuno ambazo hufichwa sana

Utapokinunua hiki kitabu utapewa ushauri toka mwanzo hadi mwisho bure kabisa,ko kwa maana hiyo nina hitaji watu kumi tu..Baada ya kufika hao watu sitakiuza mpaka mda mwengne.
Hicho kitabu kinapatikana kwa njia ya EBOOK tunakutumia kwa njia ya whatsapp..Jinsi ya kukipata tuma message au piga simu kwa namba 0769550328. 


 
HUDUMA AMBAZO TUNAZITOA

1.Ushauri wa kitaalamu kuhusu kilimo Cha matikiti kutoka uchaguaji wa mbegu hadi kuvuna.

2.Ushauri jinsi ya kupambana na visumbufu shambani mfano wadudu,panya,magonjwa.

3.Ushauri wa gharama za ulimaji wa zao la tikiti kwa wale ambao hawajai kulima

4.Kumtembelea mkulima shambani ili kutoa ushauri kwa jinsi shamba linavyoonekana

5.Kutoa msaada kwa upatikanaji wa pembejeo Kama mbolea,sumu ya wadud na ukungu.

6.Huuzaji wa mitego ya kudhibiti inzi wa matikiti

 Lengo kubwa ni kulima kilimo chenye tija ambacho kinaambatana utoaji wa tikiti kubwa na Bora

LAKINI KUNA GHARAMA KUHUSU USHAURI WA KILIMO CHA MATIKITI TOKA MWANZO HADI MWISHO YA KILIMO HICHI....MALIPO YATAKUWA AINA MBILI AMBAYO NI  KIINGILIO  Sh25,000 NA MWISHO WAKATI WA MAVUNO SH25000.

KAMA UMEPATA SHIDA YOYOTE SHAMBANI NA UNATAKA SULUHISHO ni Sh 10,000 hii ni kwa wale ambao hatujaingia nao mkataba.

MALIPO

Yafanyike kwa  NMB account namba 22 110 034 067 AMAN JOSEPH KINGU


MAWASILIANO

kwa whatsapp au njia ya kawaida

Mtaalamu OBEDI KAYANGE  

PIGA  0769550328

Whatsapp 0769550328


Mtaalamu AMANI KINGU   

0766298379







Comments

  1. Ahsantee Sana, ama kweli nimejifunza kitu hapa,

    ReplyDelete
  2. Kwakweli ubarikiwe sana. Sijawahi kuona mchanganuo na Maelezo Makini kama haya Kuhusu kilimo. Kuanzia upandaji mpaka uvunaji umeeleweka vizuri kabisa. Nakushukuru sana kwa Elimu Hii, kazi nzuri sana. Ninakwenda sasa kufanya kimatendo shambani kwangu Arusha.

    ReplyDelete
  3. Asante sana mkuu, sasa kazi naenda kuifanya

    ReplyDelete
  4. Aiisee asanteni Sana kwa ushauli na darasa nzuri mno nami nimetosheka vya kutosha

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

KILIMO CHA MATIKITI MAJI toleo la pili

JIFUNZE KUHUSU KILIMO CHA KISASA CHA MATUNDA