JIFUNZE KUHUSU KILIMO CHA KISASA CHA MATUNDA
KILIMO CHA MATUNDA
Kilimo
ambacho kinakua kwa kasi sana kwa Tanzania na kwa Dunia kiujumla,Uhuhitaji wa
matunda kwa matumizi ya nyumbani na kiwandani huongezeka mara dufu kadri siku
zinavyoenda.Hichi kilimo kinahusisha miti ambayo huchukua miaka miwili hadi
mitatu mpaka kufikia mavuno.
Kilimo
cha matunda kinaumuhimu mkubwa sana kama
i. Kuongeza kipato
endelevu kwa mkulima
ii.kuongeza uhakika
wa chakula
iii.kupungua hewa ya
ukaa,
iv.kupunguza
ongezeko la joto, na kuboresha mkusanyiko wa mawingu ya mvua,
v. kuimarisha utunzaji
wa maji aridhini katika maeneo ya mashambani
vi. Hakina gharama
kubwa katika utunzaji
Hivyo basi elimu ya utunzaji mzuri wa bustani za matunda ni muhimu ili kuweka mazingira mazuri ya uoto wa kijani, kuhifadhi ardhi na kujihami na mabadiliko ya tabia nchi.
SIFA
ZA MATUNDA
§ Ukubwa wa tunda/ Uzito wa tunda
§ Utamu wa tunda
§ Kiwango cha mafuta (parachichi)
§ Udogo wa mbegu (Embe na parachichi)
§ Rangi ya ganda la tunda likiwa bichi au
linapoiva (embe na parachichi)
§ Urahisi wa kumenya ganda (parachichi)
§ Ugumu wa ganda kuvumilia kubonyezwa
(parachichi, chungwa)
§ Unene wa ganda (parachichi, chungwa)
§ Kuwa au kutokuwa na mbegu (chungwa)
SIFA
ZA MITI YA MITUNDA
§ Kuzaa mapema
§ Matunda kuwahi kuiva/kukomaa ndani ya msimu
§ Mti kuwa mkubwa
§ Mti kuzaa mara mbili au zaidi kwa mwaka
§ Kuvumilia ukame
§ Kuhifadhi matunda kwa muda mrefu baada ya
kukomaa/kuiva bila kudondoka
Zifa
hizi na nyinginezo huwa na maana kwa jamii hasa kwa sababu za kibiashara na
matumizzi. Kwa mfano,miembe dodo ambayo huwa na matunda makubwa huuzwa kwa bei
ya juu, hivyohutumika kama zao la biashara zaidi kuliko kuliwa
nyumbani/shambani, kama ilivyo kwa embe aina ndogo ndogo kama sindano. Aina
ndogo za embe zinapoiva hata watoto wanazipata kwa urahisi na kula. Kwa upande
mwingine, embe ndogo kama sindano, huzaa matunda mengi, hata wakati wa hali
mbaya a hewa.
AINA
YA MICHE YA MATUNDA
1. Miembe § Tomyy § Red India § Apple Mango § Dodo § Bolibo § Alphonso § kenti 2.Ndizi |
3.Parachichi 4.Topetope 5.Fenesi 6.Pesheni 7.Komamanga 8. Mbilimbi 9. Chenza 10.Ndimu |
11.Papai § Malkia F1 § Calphonia |
12. Tende 13. Sherisheri 14. Zaituni |
15.Michungwa |
|
16.Limao 17.Tini 18.peasi |
|
19.Pera |
|
UCHIMBAJI
WA MASHIMO NA KUPANDA
Shimo
linashauriwa liwe refu wastani kwa 0.6mX0.6mX0.6m(UPANA 0.6mX0.6m,UREFU 0.6m),
hata chini ya hapo kulingana na hali ya udongo (rutuba, aina ya udongo nk).
Wakati wa uchimbaji wa mashimo haya, udongo wenye rutuba (wa juu) ni lazima utenganishwe na udongo wa
chini. Weka udongo wa juu sehemu ya mwinuko na wa chini sehemu ya mteremko ili
kukumbuka. Mashimo haya huandaliwa/huchimbwa halafu hujazwa debe moja/ndoo ya
lita 20 za mboji hususani maeneo yaliyo na rutuba dhaifu. Unaweza kuweka debe
moja hadi tatu za samadi au mboji iliyoiva kikamilifu kutokana na aina na
rutuba ya udongo.
Mbolea ambayo haijaoza vizuri ni hatari kwani yaweza kuunguza mizizi ya
miche.Mara nyingine hulazimu kuandaa shamba na kupanda siku zijazo. Kama hili
litatokea, mkulima anashauriwa kuweka mambo (kijiti) katikati ya shimo kama
alama ya katikati ya shimo hivyo kurahisisha upandaji wakati ufikapo.
Kwa kuzingatia nafasi za kila mche katika ekari unapata idadi ya miche
AINA MCHE |
IDADI YA
MCHE |
Embe |
miche 64 |
Parachichi |
miche 64 |
Chungwa |
miche 200 |
Cheza |
miche 200 |
Ndimu |
miche 200 |
limao |
miche 200 |
topetope |
miche 200 |
fenesi |
miche 200 |
UPANDAJI
WA MICHE
Wakati
wa kupanda, ni lazima kukata mizizi yote iliyotokeza nje ya kiriba kabla ya
kutoa mche. Hii husaidia ukuaji wa mizizi mipya na kurahisisha utoaji wa mche
kwenye mfuko. Toa mche taratibu na hakikisha kikulia mmea hakitengani na
mizizi. Miche hupandwa kwa usawa wa kina kilekile kama ilivyokuwa kitaluni.
Epuka kupanda miche chini zaidi ya ilivyokuwa kwenye kiroba kwani
yaweza kusababisha kushambuliwa na magojwa na kufa. Sehemu iliyobebeshwa ni
lazima iwe juu ya ardhi kwa kiasi kisiasi cha 10-20 sm. Sehemu hii haitakiwi
ifike kwenye udongo. Ikitokea hivyo, kitawi kilichobeshwa kinaweza kutoa mizizi
yake na kisha kuharibu maunganisho. Pia sehemu hii ni rahisi kushambuliwa na
wadudu wasababishao magonjwa Shimo hufukiwa hadi kufikia sehemu uliyotenganisha
mizizi na shina kwa kushindilia udongo.
Upandaji unashauriwa kufanyika mwanzoni
mwa mvua ndefu za masika ili miche iweze kupata maji ya kutosha kabla
kiangazi kuanza. Tengeneza Kuzunguka miche iliyopandwa visahani na kuvifunika
na majani makavu ili kurahisisha umwagiliaji ikiwa ni kipindi cha kiangazi,
kuzuia unyevu usipotee na kupunguza joto ardhini. Weka miti ya kuizuia miche
isianguke hasa kama miche inagusa ardhi. Kwa ujumla, inashauriwa kuwa na kinga
dhidi ya upepo/kimbunga. Hii inasaidia kuepusha kuvunjika kwa miche michanga na
hata miti mikubwa hususan wakati inapokuwa imezaa. Kwa maeneo yenye upepo
mkali, ni vizuri kuotesha miti ya kuzuia upepo mapema mwaka 1-2 kabla ya
kuotesha miche yako. Ni muhimu sana kumwagilia kikamilifu miche yako punde
baada ya kuipanda shambani hata kama dalili zinaonesha kuna uwezekano wa mvua kunyesha.
BAADA
YA KUPANDA
Umwagiliaji.
Utunzaji wa miche baada ya kupanda ni kama ulivyo kwa miti mingine ya matunda.
Umwagiliaji wakati wa kiangazi ni muhimu sana. Maji kiasi cha lita 15-20 kwa
kila mche kwa wiki huchukuliwa kama kiwango kizuri ila inategemeana na hali ya
hewa na aina ya udongo(utaruhusiwa
kumwagilia kwa mara nyingine pindi unyevu wa udongo unapopotea). Kuweka
maji mengi sana kwenye visahani vya miche yaweza kusababisha madhara sawa au
zaidi ya yale ya kuweka maji yasiyotosheleza. Kila mara angalia unyevu uliopo
kabla ya kuweka maji shambani na epuka kuweka maji kiasi kwamba yanatuama
kwenye visahani.
Kuwekea matandazo
Ni vizuri kutandaza majani makavu kuzunguka miche. Hii ni muhimu kuhifadhi unyevu na kuzuia magugu kuota. Matandazo haya ni muhimu yasigusane na miche ili kupunguza athari za mchwa pamoja na kuepusha unyevu wa muda mrefu kwenye shina ambao huweza kuleta magonjwa.
HUDUMA AMBAZO TUNATOA
i.
UUZAJI WA MICHE
YA MATUNDA YA MDA MFUPI
ii.
MAELEKEZO YA
JINSI KUANZISHA SHAMBA KWA AJILI YA KILIMO CHA MATUNDA
iii.
KUTEMBELEA
MASHAMBA YA MATUNDA KWA KUTOA USHAURI NA HUDUMA NYENGINEZO
TUNAPATIKANA KARIBU NA CHUO
KIKUU CHA KILIMO SOKOINE (SUA) MOROGORO,BARABARA YA BOMA(BOMA ROAD)…KWA
MAHITAJI YA MICHE POPOTE TUNATUMA NDANI YA TANZANIA
MAWASILIANO
PIGA 0769550328
Whatsapp 0769550328
mnavyo vitabu vinavyoelekeza kufanya grafting?
ReplyDeleteNikihitaji kitabu naweza kukipata au hajaviandaa nipo dodoma
ReplyDelete