KILIMO CHA MATIKITI MAJI toleo la pili
UTANGULIZI
Matikiti maji ni tunda
kubwa la mviringo ambalo linastawi vizuri katika maeneo ambayo ardhi yake
aitwamishi maji kwa mda mrefu. Matikiti maji ni mojawapo ya jamii aina ya
matunda au mbogaboga inayotambaa. Mimea hii inapatikana katika kundi
linalojumuisha mimea mingine kama kama matango,maboga na maskwash. Zao la
tikitiki maji ni mojawapo ya zao ambalo lina faida kubwa sana ukilinganisha na
mazao mengine kwa muda mfupi.Kuna aina mbili za matikiti maji moja tikikiti
lenye mbegu na lisilo na mbegu.
Tikiti maji linahitaji
vitu vitano muhimu ili uweze kuzalisha kwa wingi kama
1.mwanga wa jua wa
kutosha kwa maana hiyo eneo linatakiwa lisiwe na kivuli
2.Uwepo wa nyuki kwa
ajiri ya uchavishaji
3.Maji ya kutosha
4.Virutubisho
5.Nafasi ya kutosha
hususani katika upandaji
Mahitaji muhimu
1.Hali ya hewa
Matikiti maji
yanahitaji kipindi kirefu cha hali ya ujoto.Kukiwa na hali ya ubaridi na mvua
nyingi ina madhara kwa tikitikimaji ambayo inasababisha ukuaji hafifu,kuchelewa
kukomaaa,ukuaji mbovu wa tunda na pia husababisha tunda kuwa na uwazi katikati.
2.Hali ya udongo
Tikiti maji linahitaji
udongo ambao hautuamish maji kwa kipindi kirefu aina ya udongo huo ni kichanga
au kichanga tifitifu…Shamba likiwa na udongo ambao unatuamisha maji kwa mda
mrefu(mfinyazi sana) husababisha ukuaji wa taratibu wa zao na pia husababisha
kupasuka kwa tunda.Hali ya uchachu kwa udongo ni pH 6 hadi 7.
3.Mbegu
Kiasi cha mbegu ni
gram 500 kwa kila eka
Uchaguaji wa mbegu
Kitu muhimu katika
mkulima ni uchaguaji wa mbegu bora,Upandaji wa mbegu ambayo haina soko
hupelekea kukosa faida pindi unapo fanya mauzo
Mbegu Bora za Matikiti
Mbegu maarufu ya
tikiti ni Sukari F1, hata hivo madukani zinapatikana nyingi bora na
tofauti tofauti kama vile:
- Y F1 – kutoka Jubaeli
- Sukari
F1 – Kutoka East Africa
seeds
- Sugar
king F1 – kutoka Africasia
- Juliana
F1 – kutoka Kiboseed
- Zebra
F1 – Kutoka Balton
- Pato
F1 – Kutoka Agrichem
Uwaandaji wa shamba
Hakikisha kuwa shamba lako limelimwa vizuri na
udongo kulainika mpaka lifikie udongo
wote hauna mabonge mabonge.
Upandaji wa tikiti maji
Panda mbegu 2 moja kwa moja katika kila shimo. Usipande
katika kitalu kwasababu miche ya mitikiti huwa ni dhaifu sana wakati wa
upandikizwaji iwapo itapandwa kwenye kitalu hivyo kupelekea kufa kwa miche
hiyo. Panda umbali wa sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa mita
1 hadi 2 kutoka shina hadi shina na mita 1.5 – 3 kutoka mstari hadi
mstari.
Zingatia: usitumie mbegu za tikiti ulilonunua (kwa ajili ya kula) kwasababu
linaweza kuwa ni chotara (Hybrid) ambayo hupelekea kushusha kiasi na ubora wa
matikiti yatakayo zaliwa kwa sababu yatakuwa ni kizazi cha pili (F2).
Katika
kilimo cha umwagiliaji
1.umwagiliaji wa kutumia mifereji
2.Umwagiliaji wa
kutumia matone
Kuweka mbolea
1.kupandia
Weka samadi kiasi cha ton
8 kwa eka kabla mlimo wa mwisho…ili kuwezesha udongo na samadi vichanganyikane.
Tumia mbolea ya dukani mfano NPK,DAP na MOP katika mda wa kupanda mbegu.
2.Kukuzia
Tumia mbolea za kukuzia ili kupata mavuno mengi
Zingatia
·
Ucheleweshaji au
uwekaji kiasi kikubwa cha mbolea za nitrojen
husababisha kuwa na uwazi katikati wa tikitiki hii utokea kwenye kipindi cha
baridi
·
uwekaji kiasi kikubwa
cha mbolea za nitrojen husababisha idadi
kubwa ya mauwa dume hupelekea matunda machache
·
KWA HILO TUNA MSHAULI
MKULIMA KUPIMA UDONGO WAKE KWANZA ILI AWEZE KUWEKA KIWANGO SAHIHI CHA
VIRUTUBISHO
Shughuli nyenginezo
1.Utoaji wa magugu
2.Kupruni(pitching)
3.Uchavishaji
4.Mavuno
Wadudu na magonjwa
Kwa kawaida zao hili halina wadudu na magonjwa mengi yanayolishambulia. Hii
hutegemeana na uchaguzi sahihi wa eneo linalofaa kwa kilimo cha zao hili pamoja
na hali ya hewa. Pamoja na hayo kuna baadhi ya wadudu ambao wamezoeleka katika
zao hili.
Wadudu wa matikiti wako wa aina mbalimbali na wanaoshambulia sehemu
wanaoshambulia majani na maua, na wengine hushambulia matunda , pia kuna
magonjwa ya fangasi ambayo hushambulia mimea. Magonjwa kama Ukungu wa unga
(powdery mildew) na wa chini (Downy mildew) na mengine yathibitiwe kabla
hayajaleta madhara kwenye mimea.Ili kujua dawa za magonjwa ni vizuri kuchukua
sampuli na kwenda nayo kwenye duka la dawa na pembejeo za kilimo ili kupata
dawa sahihi. Dawa aina ya Mancozeb inaweza kutumiwa kuthibiti ugonjwa magonjwa
hayo hapo juu.
Vilevile matikiti hushambuliwa na wadudu ambao hukaa katika majani, maua na
matunda.
Dawa aina ya abernil,ninja,dudu all,actara,farmerguld itasaidia kuua wadudu wa
majani, maua na matunda.
Vidukari: Wadudu hawa ni moja ya wadudu waliozoeleka kwenye matikiti,
hushambulia sana zao hili na mara nyingi wasipodhibitiwa mapema Kabla ya
kupanda hakikisha kuwa udongo una joto la wastani wa nyuzi joto 70°C. Unaweza
kupanda kwa kutumia jembe la mkono au reki. Fukia mbegu kwenye mashimo kwa
kutumia udongo laini na shimo lisiwe na kina kirefu, liwe na wastani wa inchi
1, ili kutoa urahisi kwa mbegu kuota.
Kwa kawaida tikiti hupandwa kwa mstari mmoja kwenye tuta lenye mwinuko wa inchi
6 na upana wa futi 4. Nafasi kati ya mche na mche iwe ni sentimita 120.
Ugonjwa
Zao hili hushambuliwa zaidi na ugonjwa wa Ubwiri unga. Ugonjwa huu ni hatari
sana na usipodhibitiwa mapema kwa kuwa hushambulia majani ya mmea, husababisha
mmea kufa baada ya muda mfupi jambo ambalo huathiri mavuno.Ni vigumu sana
kuzalisha zao hili wakati wa msimu wa mvua, hivyo inashauriwa kupanda wakati wa
kiangazi. Hali hii itasaidia mazao haya kustawi vizuri, ikiwa ni pamoja na
kuepuka matunda kuoza kutokana na mvua kuwa matunda ya tikiti hukaa chini
kwenye udongo.
Uvunaji Matikiti
Kabla ya kuvuna matunda ni vema kwanza kujua kuwa matikiti huchukua takribani
miezi mitatu mpaka mitano toka inapopandwa mpaka kukomaa. Hii hutegemea na aina
ya matikiti yenyewe. Tikiti lililo komaa linaatakiwa na mwonekano wake huwa
kama ifuatavyo;
Rangi ya mng’ao hupotea Upande wa chini wa tunda huanza kuwa na rangi ya njano.Pia
kikonyo juu ya tunda hukauka kabisa na kuwa kijivu. Ila njia nzuri ni kuyapiga
kwa kiganja na kusikiliza mlio wake unakuwa kama mlio wa ngoma.Tumia kisu
wakati wa kuvuna matikiti, yabebwe na kuhifadhiwa vizuri kwenye makasha tayari
kuuzwa au kwa matumizi binafsi
Sio ugonjwa lakini ni tabia yaki phisiolojia
1.Shingo ya chupa
2.Kunyauka kwa kitako
3.Kupasuka kwa tunda
4.Michirizi ya rangi nyeupe
UKITAKA MAELEZO ZAIDI TUNA KITABU CHA KILIMO CHA TIKITIMAJI AMBACHO KINAPATIKANA KWA BEI YA PUNGUZO..WASILIANA NASI KWA NAMBA HIZO HAPO CHINI
MAWASILIANO
kwa whatsapp au njia ya kawaida
Mtaalamu OBEDI KAYANGE
PIGA 0769550328
Whatsapp 0769550328
Mtaalamu AMANI KINGU
0766298379
Barua pepe
KARIBU SANA
kilimo ni chetu sote
Hongera sana kwa maelezo mazuri, karibu shambani utushauri zaidi tuweze kupata mazao mengi zaidi ili tujenge uchumi wetu na wa nchi kwa ujumla
ReplyDeleteASANTE MKUU KARIBU SANA
DeleteNakubl boss wangu mr.fusalium kaz nzur bravoo broo
ReplyDeleteNimeupenda Sana taaluma yako uko vzr sana
ReplyDelete