KILIMO CHA MATIKITI MAJI toleo la pili
UTANGULIZI Matikiti maji ni tunda kubwa la mviringo ambalo linastawi vizuri katika maeneo ambayo ardhi yake aitwamishi maji kwa mda mrefu. Matikiti maji ni mojawapo ya jamii aina ya matunda au mbogaboga inayotambaa. Mimea hii inapatikana katika kundi linalojumuisha mimea mingine kama kama matango,maboga na maskwash. Zao la tikitiki maji ni mojawapo ya zao ambalo lina faida kubwa sana ukilinganisha na mazao mengine kwa muda mfupi.Kuna aina mbili za matikiti maji moja tikikiti lenye mbegu na lisilo na mbegu. Tikiti maji linahitaji vitu vitano muhimu ili uweze kuzalisha kwa wingi kama 1.mwanga wa jua wa kutosha kwa maana hiyo eneo linatakiwa lisiwe na kivuli 2.Uwepo wa nyuki kwa ajiri ya uchavishaji 3.Maji ya kutosha 4.Virutubisho 5.Nafasi ya kutosha hususani katika upandaji Mahitaji muhimu 1.Hali ya hewa Matikiti maji yanahitaji kipindi kirefu cha hali ya ujoto.Kukiwa na hali ya ubaridi na mvua nyingi ina madhara kwa tikitikimaji ambayo inasababisha ukuaji haf...