UMUHIMU WA MTI WA MPERA NA MATUNDA YAKE KIAFYA
MTI wa mpera ni miongoni mwa miti ya matunda inayofahamika na wengi hapa nchini. Mti huu hutoa matunda yanayofahamika kama mapera. Asili ya mti huu ni Amerika ya Kati na Kusini licha ya kuwa siku hizi unapatikana sehemu mbalimbali nchini na duniani kote. Mmea huo kama ilivyo mimea mingine ya matunda, hustawi zaidi katika hali ya hewa ya kitropiki. Hapa nchini Tanzania mti huu unasadikika uliletwa na wakoloni waliotoka mashariki ya mbali waliokuja Afrika kwa madhumuni mbalimbali ikiwemo suala la kueneza dini ya Kiislamu na Kikristo. Mapera ni miongoni mwa matunda yenye kiwango kizuri cha vitamin C pamoja na vitamin A na inaelezwa kuwa kiwango cha vitamin C kinachopatikana ndani ya pera ni mara nne ya kiwango cha vitamin hiyo kinachopatikana kwenye chungwa. Pia mapera yamesheheni virutubisho mbalimbali ikiwa ni pamoja na vitamin B2, E na K pamoja na madini ya chuma, ‘copper’, ‘potassium’ na ‘manganese.’ Kwa mujibu wa utafiti uliowahi kuchapishwa na Jarida la Journal of Human H...