Embe ni zao lenye fursa kubwa sana ya kumwinua mjasiriamali
Kwa ufupi
Kampuni ya
matunda ya Natureripe ya Kilimanjaro yenye makao yake makuu jijini Dar es
Salaam inasema embe ni zao ambalo lina fursa za kumuinua mtu kiuchumi tena kwa
haraka bila kutumia nguvu.
Ni ajabu
kuona kuwa Watanzania wengi wamekuwa hawaweki kipaumbele kwenye kilimo cha
embe. Wengi wanapenda kilimo cha kahawa, pamba, korosho, lakini embe hapana.
Hali hiyo
imetokana na kilimo kukosa tija, na kutokuwapo kwa soko la uhakika la maembe.
Kutokana
na hali hiyo maembe mengi yanaozea mashambani kwa kukosa soko la uhakika na
kusababisha wengi kutokutoa kipaumbele katika zao hilo.
Kampuni ya
matunda ya Natureripe ya Kilimanjaro yenye makao yake makuu jijini Dar es
Salaam inasema embe ni zao ambalo lina fursa za kumuinua mtu kiuchumi tena kwa
haraka bila kutumia nguvu.
Embe lina
soko kubwa
Mkurugenzi
wa Natureripe, Fatma Riyami anasema embe ni zao lenye soko kubwa duniani na
linaweza kumwingizia mtu fedha nyingi kwa kipindi kifupi.
“Tofauti
na mazao mengine, unawekeza fedha kidogo kwenye uzalishaji wa embe, lakini
unapata fedha nyingi kwa mkupuo,” anasema Riyami.
Riyami
anasema siyo aina zote za embe zina soko bali zenye soko kubwa duniani ni zile
ambazo hazina nyuzinyuzi.
Embe nyingi
zinazozalishwa nchini zina nyuzinyuzi nyingi ambazo hazina wanunuzi kwenye soko
la kimataifa kwa sababu zinakwama kwenye meno na kusababisha shida ya kuzitoa.
Anasema
mbegu ambazo hazina nyuzinyuzi tayari zimeingizwa nchini na kampuni yake na
wanaziuza kwa mkulima yeyote anayezihitaji.
“Uzuri wa
embe hizi ni kwamba zina zaa baada ya miaka mitatu tangu zilipopandwa na
huzaa kwa wingi kama zinatunzwa vizuri,” anasema.
Anasema
mti mmoja wa embe una uwezo wa kuzaa kiwango cha embe zisizopungua 300 kwa
msimu mmoja.
Kwa
kawaida mbegu hizo zisizo na nyuzi zipo za aina tano ambazo ni Apple, Kent,
Keitt, Palmel, na Tomy Atkinsi.
Mbegu hiyo
inapandwa umbali wa mita nane na kwamba kwenye ekari moja inapandwa miche 64.
Katika
shamba la maembe, yanaweza yakachanganywa mazao mengine ya muda mfupi kama vile
mananasi, mipapai, matikiti maji, na jamii za mbogamboga.
Anasema
kadri mwembe unavyokuwa, matawi yanapaswa kupunguzwa ili yasirefuke na mkulima
avune matunda ya mti huo bila kupanda mtini.
Kuhusu
mbolea anasema inategemea ushauri wa kitaalamu kulingana na aina ya udongo wa
shamba linalotumika.
Pia dawa
ni muhimu kwa ajili ya kuua wadudu wanaosababisha maua kupukutika au matunda
kuoza.
Anasema
wakulima watakaofika kununua mbegu hizo watapewa elimu ya kilimo hicho, ushauri
na namna ya kupata masoko wakati wa mavuno.
Kampuni ya
Natureripe licha ya kulima embe pia inanunua embe za wakulima na kuuza katika
masoko ya kimataifa hasa nchi za Mashariki ya Kati.
Aina za miti ya maembe
Zipo aina nyingi za embe, hapa, tumeelezea chache tu, ambazo ni nzuri kibiashara.
apple: Aina hii ya maembe asili yake ni pwani ya Kenya. Ina rangi nzuri ya njano au rangi ya chungwa inapoiva, matunda haya ni ya kiwango cha kati na kubwa, yenye muonekano wa mviringo na ngozi laini, na hayana nyuzi kabisa. Aina hii ina soko zuri, na inazaa sana
Kent: Aina hii ina rangi ya kijani na njano nzuri inayovutia kwenye sehemu ya juu. Maembe haya ni rojo rojo na nyama yake ni ya njano iliyokolea na hayana nyuzi nyuzi, yana ladha nzuri sana. Miti yake ina umbo kubwa iliyo nyooka kwenda juu na ni mazuri kwa kuuza nje ya nchi.
Tommy Atkins: Aina hii imekuwa maarufu sana kibiashara. Maembe haya ni magumu kiasi, yana njano iliyokolea, maji maji ya kiasi, na nyuzi za kiasi, pamoja na harufu nzuri. Ni aina nzuri kwa kuuza nje ya nchi kwa kuwa inastahimili kukaa muda mrefu bila kuharibika. Aina hii pia inaweza kukabiliana na ugonjwa wa kimamba na madoa madoa ya kubambuka.
Keitt: Aina hii ina ubora wa pekee katika kuhifadhiwa na inaweza kuachwa juu ya mti kwa muda mrefu hata baada ya muda wa kawaida wa msimu kupita. Matunda yake ni makubwa, na yanakuwa na rangi ya kijani na njano, au nyekundu iliyofifia. Ina kiasi kikubwa cha weupe, au njano/ nyekundu kwenye ganda lake ambalo ni nene na gumu. Tunda lake lina umbo kama yai na lenye mviringo mzuri, na halina mdomo mgumu, kikalio chake ni cha mviringo. Mti wake una umbo la kati na huwa na matawi marefu yanayojikunja, na yana nafasi inayoruhusu kuonekana vizuri, na yana uwezo wa kubeba uzito mkubwa. Aina hii ina soko zuri, na inazaa sana na pia ina uwezo wa kukabiliana na ugonjwa wa madoa doa ya kubambuka.
Faida ya
kulima embe
Katika
msimu uliopita walinunua embe moja kutoka kwa wakulima kwa Sh100.
“Ina maana
kwamba kwa mkulima mwenye shamba la ekari moja lenye miche 64 ambalo limezaa
maembe 300 kwa mti mmoja. Mkulima atapata Sh1.9 milioni,” anasema Riyami.
Anasema
ekari moja inagharimu Sh300,000 kupanda mpaka kuvuna na mkulima kupata faida ya
Sh Sh1.6 milioni.
Kampuni
hiyo pia inasindika matunda ya embe ili kutengeneza bidhaa mbalimbali.
“Hivi sasa
tunatengeneza chachandu inayotokana na embe. Tunazo aina tatu zinazojulikana
kama Mango Pilipili, Mango Zodo na Mango Pickle,” anasema Riyami.
Pia wana
mpango wa kusindika embe kwa ajili ya kutengeneza juisi ambazo hazina
kemikali.
Wakati wa
maonyesho ya kuonja embe yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa mwaka
huu, Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima wa Embe nchini(Amagro) Burton Nsape
anasema kuwa chama hicho kinawasaidia wakulima wa embe kujipatia kipato kupitia
zao hilo na pia hutoa elimu kwa wanachama wake kuhusiana na kilimo cha embe.
Nsape
anasema changamoto kubwa inayowakabili wakulima wa embe nchini ni ukosefu wa kusafirisha
kitaalamu kutoka mashambani hadi sokoni.
Karibu ujipatie Miche bora ya miembe ya kisasa, aina hizo hapo juu na nyingne.
Pia tunayo miche ya matunda mengine kama Papai, parachichi, Michungwa, Migomba. Miche yote hii ni ya kisasa na ni ya muda mfupi.
Pamoja na Miche utapatiwa ushauri wa kitaalamu.
Vitalu vyetu vya miche vinapatikana Morogoro. Kwa wateja wa mikoani tunatuma, na miche inafika salama kabisa
Mawasiliano: Simu 0769255000
Tazari tunaomba namba za mawasiliano yenu pamoja na anwani
ReplyDelete0769255000/0620302031
DeleteMaelezo yako nimeyapenda, naomba uongeze bei za miche ili tujue gharama zako.
ReplyDeleteNitawatembelea na kununua Miche
ReplyDelete