Kilimo Bora Cha Matikiti Maji
Matikiti maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wastani. Zao hili lina wapatia watu shughuri za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi. Matikiti maji ni mojawapo ya jamii aina ya matunda au mbogaboga inayotambaa. Mbegu Bora za Matikiti Mbegu maarufu ya tikiti ni Sukari F1 , hata hivo madukani zinapatikana nyingi bora na tofauti tofauti kama vile: Arashani F1 – kutoka Syngenta Sukari F1 – Kutoka East Africa seeds Sugar king F1 – kutoka Africasia Juliana F1 – kutoka Kiboseed Zebra F1 – Kutoka Balton Pato F1 – Kutoka Agrichem MAHITAJI YA TIKITIMAJI Tikiti linakua vizuri katika udongo unaoshika maji vizuri lakini yasio tuama na kuruhusu mzunguko mzuri wa hewa na maji.Udongo wenye pH 5.8-6.6.pia kama pH ni ndogo tutakushauri cha kufanya ili iweze kuwa nzuri na ya kiasi kwa ajili tikitimaji....