KILIMO CHA BUSTANI AMBACHO HAKIHITAJI ENEO KUBWA
Habari ndugu msomaji wa wetu wa makala za kilimo, Natumaini tunaendelea vizuri na mapambano ya kila siku. Leo tutaanza kujifunza kilimo cha bora cha mboga mboga ambacho:
na tutaanza kufahamu vitu vya msingi kwanza, na natumaini ukimaliza mfululizo wa makala hizi utakua mkulima hodari wa nyanya. Kila kitu lazima kiwe na msingi imara, karibu tujifunze wote:
- hakiitaji eneo kubwa
- huzalisha mboga kwa wingi
- hautaji kuwa na maji mengi ya umwagiliaji
- Inapunguza utumiaji wa kemikali za viwandani
- Gharama za uhitaji wa mboga za majani.
- inatumia nafasi ndogo na kutoa kiasi kikubwa cha mboga mboga.
na tutaanza kufahamu vitu vya msingi kwanza, na natumaini ukimaliza mfululizo wa makala hizi utakua mkulima hodari wa nyanya. Kila kitu lazima kiwe na msingi imara, karibu tujifunze wote:
Vifaa:
Udongo, Kokoto (mawe madogo madogo), Gunia, mchanga/Pumba za mpunga (Rice husk), Mbole ya samadi iliooza vizuri, mti/mbao na kopo dogo (sadolini).
Udongo - Kwa ajili ya kuwezesha mmea kusimama, pia kupatia virutubisho mmea
Mchanga/Rice husk - Kusaidia mizizi kupita kwa urahisi, pia kuweka mazingira mazuri ya hewa na maji katika udongo yaani mzunguko wa maji na hewa.
Kokoto - Kusadia maji kupita ndani ya gunia toka juu hadi chini
Mbolea ya samadi - Kutoa virutubisho kwa mmea
mti/Mbao - Kusaidia gunia lako kusimama vyema/ imara
Hatua za utengenezaji
(i) Changanya udongo wako na mchanga/rice husk pamoja na mbole katika uwiano wa 5:2:1.
5 udongo, 2 samadi, 1 Mchanga/rice husk.
(ii) Toboa kopo lako na ondoa kitako ili kuweka uwazi pande zote mbili (juu na chini)
(iii) Weka mti/ubao katikati ya gunia ukiuchimbia ardhini kisha weka kopo lako katikati ya mti/mbao hiyo na lijaze kokoto
(iv) Weka udongo uliochanganywa vizur kwenye gunia lako ukilizunguka kopo lenye kokoto hadi kufikia kimo cha kopo. Baada ya hapo ondoa kopo na hakikisha kokoto zinabaki zikizungukwa na udongo.
(v) Weka kopo juu ya kokoto zilizozungukwa na udongo kisha, lijaze kopo hilo na kokoto, rudia kujaza udongo ukilizunguka kopo hadi kimo cha kopo hilo. Endelea kufanya hivyo (kama hapo juu) hadi pale gunia lako litakapokuwa limejaa.
(vi) Toboa gunia kwa kuweka matundu kuzunguka gunia kwa ajili ya kupandia katika umbali sawa (inategemea na aina ya mboga)
(vii) Hapo utakuwa tayari kupanda mbegu zako ama mche wa mboga aina yoyote juu na pembeni ya gunia lako
AINA YA MBOGA
Mboga aina ya letuce
Mboga aina ya sukumawiki zikiwa zimepandwa kwenye gunia
Uangalizi.
- Mwagilia mboga yako mara baada tu ya kupanda na kuendelea ikitegemeana ni aina gani ya mboga.
- Unapoona magonjwa hasa fangasi wa ukungu na wadudu wa mboga unaweza tumia dawa zisizo za kikemikali za viwandani kama vile majani ya pilipili kichaa, mwarobaini na tumbaku.
- Mboga kama sukuma wiki waweza vuna mara kwa mara, kazi yako ni kumwagilia tu.
- unatakiwa kubadilisha udongo wako kwa muda mfano. baada ya mavuno 2 ili kuakikisha mboga zako zina pata virutubisho ya kutosha.. ( Hii inategemeana ni aina gani ya mboga)
Muhimu: Ukitumia miche kwa siku tatu/mbili za mwanzo usije ogopa kuona miche yako imelala endelea kuimwagilia itasimama tu. Pia katika umwagiliaji hakikisha unamwaga maji katika kati ya guni pale kulipo na kokoto ili kuhakikisha maji yanasamba ndani ya gunia hadi chini.
KWA WALE WANAOHITAJI MAFUNDISHO HAYO NYUMBANI KWAAJILI YA KILIMO HIKI WANITAFUTE KWA NAMBA HIZO CHINI NA NIJE NYUMBANI KWAKO KUKUFUNDISHA KIVITENDO. namba 0769255000
Comments
Post a Comment