KILIMO CHA VITUNGUU
Utangulizi
Kitunguu ni mojawapo la zao linalimwa
kwa wingi na pia linawatumiaji wa kila siku nchini na nje ya nchi.
Linachukua nafasi ya pili baada ya nyanya. Kitunguu kinatumika katika
kachumbari, kama kiungo kwenye kitoweo kama vile Samaki, nyama, mboga za mahani
n.k. Majani ya vitunguu hutumika kama mboga. Vitnguu pia hutumika kuandalia
supu.vitunguu vimetofautiana kwa rangi(nyekundu,njano na nyeupe),umbo(mviringo
na bapa) na radha(tamu na punget).
Mahitaji
muhimu kwenye kilimo cha vitunguu
1.Hali ya hewa
Kitunguu hustawi vizuri kwenye mvua
kiasi mm 500 had mm 700.Hali ya ujoto eneo hilo liwe na ujoto kiasi ambacho
kinaweza kuwa nyuzi za joto 15 hadi 30,joto la kawaida sana.Endapo joto
likazidi nyuzi joto 30 kitunguuu hukomaa
kwa haraka kabla ya mda wake na pia kupelekea umbo kuwa dogo na mavuno kupungua.Endapo
joto likawa chini sana inasababisha ukuaji wa taratibu na kitunguuu kuanza
kutoa mauwa kabla ya wakati na pia hali ya baridi hupelekea magonjwa ya majani.
2.Udongo
Kitunguu kinahitaji udongo wenye rutuba
ambao hautwamishi maji kwa mda mrefu ambao ni kichanga tifutifu na uchachu wa udongo unatakiwa pH 6 hadi 8.
Uchaguaji
wa mbegu bora
Kama wataalamu wa kilimo tunashauri
mkulima anunue mbegu bora kutoka kwenye kampuni yenye kuaminika.Mbegu bora
inamanufaa makubwa sana kwa sababu ndo chanzo cha ongezeko la mavuno shambani
kwako.
Kuna aina nyingi za mbegu za vitunguu
lakini mimi katika makala yangu nitaeleza mbili tu ambazo ni RED BOMBAY na RED
CREOLE
1.Red Bombay
i.
Ni mbegu ambayo inafanya vizuri zaidi maeneo
yenye hali ya ukavu na ujoto
ii.
Inatoa vitunguu kuanzia size ya ndogo
hadi ya kati,rangi ya zambarau nyekundu
iliyo kolea na umbo la dunia
iii.
Inakomaa siku 150 baada ya kupandikiza
kutoka kwenye kitalu
iv.
Inatoa mavuno wastani wa kilo 16000 kwa ekari
2.Red creole
i.
Inatoa vitunguu rangi ya nyekundu na umbo la bapa mzunguko
ii.
Inakomaa siku 150 baada ya kupandikiza
kutoka kwenye kitalu
iii.
Inakaa mda mrefu gharani au hairabiki
haraka baada ya kuvunwa
iv.
Inatoa mavuno wastani wa kilo 16000 kwa ekari
Uwandaaji
wa shamba
Hakikisha
kuwa shamba lako limelimwa vizuri na udongo kulainika mpaka lifikie udongo
wote hauna mabonge mabonge.
Uwandaaji wa kitalu
Weka tuta lenye upana wa mita 1 changanya na mbolea ya samadi
kilo 20 kwa mita 1 za mraba na pia weka na mbolea ya kupandia DAP/TSP gram 20
kwa mita 1 za mraba.Na pia nafasi kati ya tuta moja na jengine ni sm50 na urefu
wa huo mfereji ni sm1 .Kiasi cha mbegu ni gram 800 hadi 1200 kwa ekari
inapandwa kwenye kitalu bila kusahau matandazo.Mbegu hutumia siku 7 hadi 10 maotea kuonekana.
Katika kuhudumia
kitalu
mwagilia kitalu chako kwa mpangilio baada maotea kuonekana,,toa matandazo,weka
kichanja kwa kila tuta ili kuzuia jua.Na pia fanya kutoa magugu,dhibiti
magonjwa na wadudu pindi dalili zinapoonekana.
Kupandikiza
1.mda wa kupandikiza
Mche unapandwa baada ya wiki 6 hadi 8 baada ya kupanda au
ukifika majani 3 hadi 5 pindi kitako kinakuwa unene kama penseli
2.Nafasi kwa kila mche
Mche unapandwa kwenye shimo la sm 2.5 hadi 3 na pia kati ya
msitari mmoja na mwengine sm30 na pia kati ya mche mmoja na mwengine sm8 hadi
sm10.
3.Njia zakupandikiza
Mwagilia kabla ujatoa mche kutoka kwenye kitalu,vuta taratibu
mche kutoka kwenye kitalu ili usiharibike,unapopanda mche usifukie udongo zaidi
ya inchi moja.
Katika kilimo cha
umwagiliaji
Kitunguu kinaitaji umwagiliaji mwepesi na wakila mara ambao upo
katika utaritibu maalumu
1.katika hatua ya ukuaji -------Umwagiliaji
wa maji mengi unatakiwa kuzuiliwa
2.katika hatua ya utungaji wa kiazi-----tunahitaji kumwagilia
maji mengi
3.katika kipindi cha
kukomaa-----tunatakiwa kupunguza au kuacha kabisa kumwagilia
Zingatia:kumwagilia
kwa mpangilio maaulumu unasaidia kuondoa tatizo la mzizi kuwa ya
pinki,inaimalisha afya ya mizizi na pia ukuaji kitunguu ulio bora.
Ukosefu wa unyevu husababisha kitunguu
kukatika au kuundwa kwa vitunguu viwili katika mmea mmoja.
Kuweka
mbolea
1.kupandia
Weka samadi kiasi cha
tan 10 hadi 16 na tumia jembe kwa ajili
yakuchanganya na samadi inatakiwa kuwekwa wiki moja hadi mbili kabla ya
kupandikiza,kitunguu kinafanya vizuri kama ukiweka samadi.
Tumia mifuko miwili ya
mbolea ya DAP/TSP au NPK kwa eka
katika mda wa kupandikiza.
2.Kukuzia
Hili tunashauri mkulima atumie njia ya kuweka karibu na mmea
lakini usigusane kuliko njia yakutawanya.Tumegawa katika vipindi viwili
Kipindi cha kwanza---hii inafanyika siku30 baada ya kupandikizwa
ambayo ni mifuko mmoja ambayo ni UREA
Kipindi cha pili----hii inafanyika siku 45 baada ya kupandikizwa
ambayo ni mfuko mwili ya CAN
Zingatia: uwekaji wa kiasi kikubwa cha nitrojeni husababisha
shingo nene na uwekaji wa mbolea umalizike kabla ya kutungwa kwa kiazi.
Fanya kupunguza udongo ili kufanya kutanuka kiazi
vizuri hii inasadia kwenye rangi ya kitunguu na pia katika kipindi cha kuvuna.Na
pia kama udongo wako ni mgumu fanya kuupunguza ili kufanya ukuaji mzuri wa kiazi.Hiii
hufanyika katika parizi ya pili na inayofuata hii ifanyike kwa mkono na pia
kuwa makini na mizizi ya kitungua kutoharibika.
Wadudu wanaoshambulia vitunguu
Kuna aina nyingi za wadudu wanaoweza kushambulia vitunguu.
Hawa wafuatao ni baadhi ya wadudu waliozoeleka kwenye zao la vitunguu.
1.Thiripi
Wadudu hawa hukaa kwenye jani sehemu inayokutana na shina.
Wadudu hawa hufyonza maji kwenye majani ya vitunguu na kusababisha majani kuwa
na doti nyeupe.
Madhara: Husababisha vitunguu kudumaa hivyo kuathiri ukuaji wake
jambo ambalo huathiri mavuno pia.
2.Kimamba
Wadudu hawa hufyonza maji kwenye vitunguu, na kusambaza ugonjwa
wa virusi. Husababisha kudumaa kwa vitunguu. Wadudu hawa ni hatari zaidi kwa
kuwa husambaza virusi vinavyoingia hadi kwenye mbegu.
3.Minyoo fundo
Aina hii ya minyoo hushambulia mizizi ya vitunguu. Hali hii
husababisha kudumaa kwa vitunguu kwa kuwa hushindwa kufyonza maji na chakula
kutoka ardhini.
4.Vidomozi
Hushambulia majani kwa kujipenyeza kwenye ngozi ya jani na
kusababisha michoro ambayo huathiri utendaji wa majani.
5.Utitiri mwekundu
Wadudu hawa hufyonza maji kwenye majani na kusababisha vitunguu
kunyauka.
6.Funza wakatao miche
Funza hawa hutokana na wadudu wajulikanao kama Nondo, na
hushambulia shina na kulikata kabisa.
Namna ya kukabiliana na wadudu hawa
Unaweza kukabiliana na wadudu hawa kwa kufanya kilimo cha
mzunguko. Usioteshe vitunguu sehemu moja kwa muda mrefu, au kufuatanisha
mazao jamii ya vitunguu kama vile leaks.
Tumia mbegu bora zilizothibitishwa kutoka kwenye kampuni
zinatambuliwa kisheria na kibiashara. Kupanda kwa wakati unaotakiwa;
vitunguu visipandwe wakati wa kiangazi. Vipandwe wakati wa majira ya baridi na
kuvunwa wakati wa joto. Tumia dawa za asili za kuulia wadudu, au dawa
nyinginezo zinazopendekezwa na wataalamu wa kilimo.
Magonjwa yanayoshambulia vitunguu
1. Purple blotch
Ugonjwa huu husababishwa na ukungu (fungus). Ugonjwa huu
husababisha mabaka ya zambarau na meusi katika majani ya vitunguu.
Ugonjwa huu hutokea wakati wa unyevu unyevu mwingi.
Madhara: Ugonjwa huu hupunguza mavuno mpaka asilimia hamsini (50%).
Kudhibiti: Unaweza kuzuia kwa
kutumia kiuwa kuvu chenye viambata Mancozeb na Difenoconazole.
2. Stemphylium leaf
blight
Hukausha majani
kuanzia kwenye ncha hadio kwenye shina.; Ugonjwa huu hutokea wakati wa unyevu
na ukungu mwingi.
Madhara: Hupunguza mavuno hadi kwa asilimia sabini na tano (75%).
Kudhibiti: Unaweza kuzuia kutumia
kiuwa kuvu chenye kiambata cha copper
3. Magonjwa ya
virusi
Ugonjwa huu husababisha vitunguu kuwa na rangi iliyochanganyika,
kijani na michirizi myeupe au njano. Vitunguu hudumaa kwa kiasi
kikubwa;Ugonjwa huu husababishwa na kimamba.
Madhara: Huathiri mavuno kwa asilimia 80 mpaka asilimia 100%.
Kudhibiti: Unaweza kuzuia
vimamba ambao ndio wanaoeneza virusi kwa kutumia dawa za kuulia wadudu
4. Kuoza kwa kiazi
Husababishwa na fangasi. Ugonjwa huu hutokea vitunguu
vikishakomaa, huku udongo ukiwa na maji maji. Vitunguu vikishakomaa
visimwagiliwe tena.
Kudhibiti: Unaweza kuzuia kwa
kuvuna mapema,fanya kilimo mzunguko,kausha baada ya kuvuna na ondoa kiazi kilicho
onyesha dalili za kuoza.
Uharibifu wa vitunguu usiotokana na magonjwa
1.kuchipua baada
ya kuvunwa
Hali hii hutokea endapo vitunguu vitavunwa kabla ya muda wake.
Endapo vitunguu havitakaushwa vizuri baada ya kuvunwa. Hali hii
husababisha uharibifu mpaka asilimia themanini (80%). Sehemu ya kukaushia
vitunguu iwe na hewa inayozunguka na mwanga wa kutosha. Vitunguu vikiwekwa
gizani huchipua kwa urahisi.
2. Muozo laini
Ugonjwa huu hushambulia vitunguu baada ya kukomaa; husababishwa
na vimelea (bacteria). Vitunguu hutoa harufu mbaya ya uozo. Kuepuka hilo
vuna kwa wakati unaofaa, hifadhi sehemu yenye mwanga na hewa inayozunguka.
Mavuno
Mavuno ya kitunguu hufanyika siku 90
hadi 150 kutegemea mbegu uliyopanda.kitunguu kinakuwa tayari kipindi majani
yamedondoka na asilimia 70 ya upande wajuu umekauka na kudondoka
PIA KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU KILIMO HICHI mfano mbegu bora,uwekaji wa mbolea,udhibiti wa magonjwa,ratiba na umwagiliaji mzuri na n.k
KWA WALE WANAOHITAJI MAFUNDISHO HAYA KWA AJILI YA KILIMO HIKI WANITAFUTE KWA NAMBA HIZO CHINI.
Kwa mawasiliano zaidi
PIGA 0769550328
Whatsapp 0769550328
Barua pepe
KARIBU SANA
Comments
Post a Comment