KILIMO CHA NDIZI



UTANGULIZI

KILIMO CHA NDIZI ili uweze kulima kibishara licha ya kuwa na changamoto za magonjwa na wadudu basi kinahitaji ufuate mbino Bora za kilimo.

Mbinu Bora za kilimo kinaendana na uchaguaji wa mbegu bora ambazo hazina vimelea vya magonjwa mbalimbali pia zenye kuimili mihangaiko yoyote itakayo tokea Kama mvua nyingi au mvua chache,baridi au joto kali na pia upepo...Pia tunalenga katika uzalishaji wa kiasi kikubwa ambacho ndo kiini cha lengo la kupanda migomba,migomba inayo itajika ni ile ambayo huzaaa kwa kiasi kikubwa ili uweze kupata kipato kikubwa.

VITU MUHIMU

Ndizi(vidole) hukaa katika makundi madogo inayoitwa kichana huwa na ndizi(vidole) 20 ambayo mkungu mmoja huchukua vichana kuanzia 3 hadi 20 kwa wastani..kutokana na Aina tofauti tofauti za migomba uzito wa mkungu  kuanzia  kilo 30 Hadi 50.

Tunaaina mbili za migomba

1.migomba ya kienyeji

2.migomba ya kisasa


1.Migomba ya kienyeji

Hiii hotolewa kutoka kwa mama..mfano mzuzu,mshare,kisukari,mkono wa tembo n.k

2.migomba  ya kisasa

Ambayo huzalishwa kwa njia ya kichupa(tissue culture) na ndio inayopendwa duniani.mfano William,Grand Naine na Cavendish.

Migomba huchukua miezi 9 Hadi 15 mpaka kufikia mavuno hii hutegemea hali ya hewa,sehemu ya joto huwai kuvunwa tofauti na sehemu ya baridi na pia migomba ya kisasa huchelewa kuvunwa tofauti na ya kienyeji.

Nafasi katika shamba ni 3 × 3 na ukubwa wa shimo ni mraba wa mita 1.katika ekari moja hutosha miche 530.

Kuna Aina ambazo 

1.huliwa kwa kuzichoma,kukaanga au kupikwa mfano mzuzu,Mshare,Matoke,Bokoboko na Mkono wa tembo.

2.huliwa Kama matunda mfano kisukari,kimalindi,mzungu na mtwike.

3.ambazo hupendwa katika masoko ya ulaya 

Grand naine,williams,jamaica,uganda green na embwailuma giant.


MASOKO

Duniani nchi inayoongoza kwa kulima migomba ni India,na Afrika ni Uganda sisi Tanzania tunashika nafasi ya 11 na pia mikoa ambayo inaongoza kwa uzalishaji Bukoba,Mbeya na Kilimanjaro.

 Soko la ndizi linahitajika mwaka mzima.na msimu wa kuanza kulima ni Sasa ambapo mvua zinaanza kunyeshA



kwa mahijati ya miche ya ndizi

mawasiliano piga 0769550328

                       Whatsapp 0769550328





Comments

Popular posts from this blog

Kilimo Bora Cha Matikiti Maji

KILIMO CHA MATIKITI MAJI toleo la pili

JIFUNZE KUHUSU KILIMO CHA KISASA CHA MATUNDA