upimaji wa udongo
KUPIMA UDONGO
upimaji wa udongo ni nini?
UPIMAJI WA UDONGO
ni kitendo cha kujua kiasi gani virutubisho vinapatikana katika udongo bila kusahau kujua uchachu wa udongo(pH).
FAIDA ZA KUPIMA UDONGO
1.Kujua kiasi gani cha mbolea kinahitajika
inamsaidia mkulima kujua anahitaji kiasi gani cha mbolea katika eneo husika..Mkulima hana haja yakuanza kukisia kukisia idadi ya mbolea.mfano unaweza kukadiria kuwa mifuko katika shamba lako inatosha mitatu kumbe unatosha mfuko mmoja.
2.Kutunza rotuba ya udongo
kiasi kikubwa kuwekwa katika udongo upelekea afya ya udongo kudhorota na kupelekea rotuba kupungua...Mfano matumizi makubwa ya UREA katika shamba inaweza kupelekea uchachu wa udongo kuwa mkubwa na hivyo kusababisha rotuba kupungua.
3.Kuongeza uzalishaji katika shamba lako
kila zao linahitaji kiasi stahili cha virutubisho,ko endapo ukaweka mbolea kwa makadirio inaweza kusababisha zao husika kupata kiwango cha chini cha kirutubisho na kusababisha mavuno kuwa machache.Na pia unaweza kuweka kiwango cha juu katika zao husika na kusababisha madhara katika mmea na kupelekea mavuno kuwa machache.
4.Kupunguza ghalama za uzalishaji
unapima udongo wako kila baada ya miaka mitano,ko ndani ya miaka mitano uantumia kiasi stahili cha mbolea kwa zao husika..kama ekari moja zao husika unatosha mfuko mmoja basi inakuwa hivyo hvyo ndani ya mda huo hii inapelekea gharama zakununua pembejeo hususani mbolea hupungua.
5.Kujua zao gani linafaaa katika shamba lako
kam ilivyo ada kuwa kila mmea unahitaji aina fulani ya virutubisho,endapo shamba lako likapimwa na kuonekana lina virutubisho husika kwa zao fulani...Inapelekea mtaalamu wa udongo kukupa ushauri ulime zao gani ili liwe na tija kwako.
Pima udongo kwa kilimo cha kisasa acha kilimo cha mazoea
Hii huduma tunatoa kuanzia ekari 5
kwa kupata huduma hii popote TANZANIA
tuwasiliane kwa namba
PIGA 0769550328
Whatsapp 0769550328
Comments
Post a Comment