Posts

KILIMO CHA MATIKITI MAJI toleo la pili

Image
UTANGULIZI Matikiti maji ni tunda kubwa la mviringo ambalo linastawi vizuri katika maeneo ambayo ardhi yake aitwamishi maji kwa mda mrefu. Matikiti maji ni mojawapo ya jamii aina ya matunda au mbogaboga inayotambaa. Mimea hii inapatikana katika kundi linalojumuisha mimea mingine kama kama matango,maboga na maskwash. Zao la tikitiki maji ni mojawapo ya zao ambalo lina faida kubwa sana ukilinganisha na mazao mengine kwa muda mfupi.Kuna aina mbili za matikiti maji moja tikikiti lenye mbegu na lisilo na mbegu. Tikiti maji linahitaji vitu vitano muhimu ili uweze kuzalisha kwa wingi kama 1.mwanga wa jua wa kutosha kwa maana hiyo eneo linatakiwa lisiwe na kivuli 2.Uwepo wa nyuki kwa ajiri ya uchavishaji 3.Maji ya kutosha 4.Virutubisho 5.Nafasi ya kutosha hususani katika upandaji   Mahitaji muhimu 1.Hali ya hewa Matikiti maji yanahitaji kipindi kirefu cha hali ya ujoto.Kukiwa na hali ya ubaridi na mvua nyingi ina madhara kwa tikitikimaji ambayo inasababisha ukuaji haf...

KINYAUSI (MNYAUKO BACTERIA)

Image
JE USHAWAHI ONA HII SHAMBANI  KAMA NI NDIO, @kilimomatunda inatoa elimu kuhusu  hili MNYAUKO BACTERIA (KINYAUSI) UTANGULIZI Ni  ugonjwa ambao husababishwa na bacteria. Bacteria huyu hushambulia sana sana familia ya mazao aina solanaceae mfano nyanya na viazi mviringo.Huu ugonjwa huweza kupunguza mavuno kwa kiasi kikubwa sana kama mkulima hata kuwa makini jinsi ya kuidhibiti.Wataalamu wa @kilimomatunda leo wamekuandalia jinsi ya kuutambua na kuudhibiti. DALILI ZA KIPEKEEE     Majani   unyauka lakini ubaki na rangi ya kijani   Ukikata kipande cha shina na kuweka ndani glass nyuepe  yenye maji  utaona ute ute unatoka kwa shina KUDHIBITI Tuna njia ambazo ni rahisi ambazo zenye matokeo chanya……kwa maelezo zaidi kuhusu hizi njia za kudhibiti ugunjwa huuu. KWA KUPIGA SIMU ILI KUPATA MAELEZO Kwa mtalaamu wetu     0769255000 KWA AJIRI YA PICHA AU VIDEO KWA ZAO HUSIKA KWA N...

UTUMIAJI WA MADAWA YA KILIMO KUTOKANA NA KISUMBUFU HUSIKA

Image
Karibu msomaji wangu katika tovuti uipendayo ya kilimo. WAHUSIKA WA @kilimomatunda WANAKULETEA HUDUMA AMBAYO ITAHUSHISHA UTAMBUZI WA KISUMBUFU(UGONJWA AU MDUDU) NA AINA YA DAWA YA KUTUMIA KATIKA SHAMBA LAKO. HII NI KUTOA DHANA YA WAKULIMA WENGI KUZITENGA BAADHI YA DAWA KUWA HAZIFANYI KAZI AU NI FEKI. UNAEZA TUMA PICHA YA ZAO LILOHARIBIWA NA VISUMBUFU KUPITIA NAMBA 0769255000  whatsapp

KANUNI SAHIHI ZA KILIMO BORA CHA MACHUNGWA

Image
 Mchungwa ni jamii ya mlimao, lakin hustawi zaidi ukanda wa pwani wenye joto kiasi, mvua zaidi na udongo wenye rutuba. Hapa Tanzania mikoa kama Pwani, Dar es salaam, Tanga, Mtwara, Lindi, na Morogoro ni maarufu kwa kilimo hiki. Pia tunda la mchungwa huliwa na binadamu ili kuongeza vitamini mwilini. HALI YA HEWA Michungwa huweza kukuzwa maeneo yenye joto na hata yale yenye baridi. Kama ilivyo kwa matunda mengineya citrus, ili kupata mazao mazuri haina budi kukuza michungwa katika joto la nyuz ijoto 15.5c – 29c. KUANDAA MBEGU Mchungwa kwa kuanzia unakusanya mbegu za mlimao kutoka katika malimao yaliyokomaa na ikiwezekana yawe yameiva yakiwa mtini, kausha mbegu zake na kasha unaweza kutolea ganda la nje ili ziweze kuota vizuri. KUANDAA KITALU Tengeneza kitalu chako vizuri kwa kutumia jembe, kisha changanya na mbolea za mboji au samadi baada ya kukauka vema mwaga mbegu zako na uzifukie kwa udongo kiasi cha nusu sentimita, kasha mwagia maji kila siku na baada ya wiki 3...

Kilimo Bora Cha Matikiti Maji

Image
Matikiti maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wastani. Zao hili lina wapatia watu shughuri za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi. Matikiti maji ni mojawapo ya jamii aina ya matunda au mbogaboga inayotambaa. Mbegu Bora za Matikiti  Mbegu maarufu ya tikiti ni  Sukari F1 , hata hivo madukani zinapatikana nyingi bora na tofauti tofauti kama vile: Arashani F1  – kutoka Syngenta  Sukari F1  – Kutoka East Africa seeds  Sugar king F1  – kutoka Africasia  Juliana F1  – kutoka Kiboseed  Zebra F1  – Kutoka Balton  Pato F1  – Kutoka Agrichem MAHITAJI YA TIKITIMAJI Tikiti linakua vizuri katika udongo unaoshika maji vizuri lakini yasio tuama na kuruhusu mzunguko mzuri wa hewa na maji.Udongo wenye pH 5.8-6.6.pia kama pH ni ndogo tutakushauri cha kufanya ili iweze kuwa nzuri na ya kiasi kwa ajili tikitimaji....