upimaji wa udongo
KUPIMA UDONGO upimaji wa udongo ni nini? UPIMAJI WA UDONGO ni kitendo cha kujua kiasi gani virutubisho vinapatikana katika udongo bila kusahau kujua uchachu wa udongo(pH). FAIDA ZA KUPIMA UDONGO 1.Kujua kiasi gani cha mbolea kinahitajika inamsaidia mkulima kujua anahitaji kiasi gani cha mbolea katika eneo husika..Mkulima hana haja yakuanza kukisia kukisia idadi ya mbolea.mfano unaweza kukadiria kuwa mifuko katika shamba lako inatosha mitatu kumbe unatosha mfuko mmoja. 2.Kutunza rotuba ya udongo kiasi kikubwa kuwekwa katika udongo upelekea afya ya udongo kudhorota na kupelekea rotuba kupungua...Mfano matumizi makubwa ya UREA katika shamba inaweza kupelekea uchachu wa udongo kuwa mkubwa na hivyo kusababisha rotuba kupungua. 3.Kuongeza uzalishaji katika shamba lako kila zao linahitaji kiasi stahili cha virutubisho,ko endapo ukaweka mbolea kwa makadirio inaweza kusababisha zao husika kupata kiwango cha chini cha kirutubisho na kusababisha mavuno kuwa machache.Na pia unaweza kuwe...